Semina ya Elimu ya Afya na Biashara Yafanyika Miligo, Kahama
Semina maalum ya utoaji elimu kuhusu Magonjwa Yasiyoambukiza ilifanyika kwa mafanikio katika Ukumbi wa Miligo mjini Kahama, mkoani Shinyanga. Lengo kuu la semina hiyo lilikuwa ni kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu magonjwa haya ambayo yamekuwa tishio kwa afya ya jamii na namna bora ya kuyadhibiti.
Katika semina hiyo, washiriki walipata fursa ya kujifunza kwa njia ya vitendo kuhusu madhara ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na mengineyo, pamoja na njia sahihi za kujikinga na kuyadhibiti.
Pia, kulifanyika utoaji wa elimu kuhusu bidhaa za BF Suma, ambazo ni virutubisho vinavyosaidia katika kuimarisha afya na kutibu baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza. Washiriki walielezwa umuhimu wa kutumia bidhaa hizi kama sehemu ya mbinu ya kujenga kinga ya mwili na kuboresha maisha kwa ujumla.
Semina hii iliambatana na elimu juu ya Biashara ya Mtandao (Network Marketing), ambapo washiriki walihamasishwa kujiunga na mtandao huu wa kibiashara kupitia kampuni ya BF Suma, ili waweze kuongeza kipato chao na kujenga uchumi endelevu sambamba na kuimarisha afya zao. Haya yote yalifanyika chini ya kampeni maalum iitwayo βLinda Afya Yanguβ.
Kampeni hii inalenga kuwawezesha wananchi kuwa na uelewa mpana kuhusu afya, kujitambua, na kujitegemea kiuchumi kwa njia halali na endelevu.